Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF Yawarudisha Waamuzi Wote Darasani

Refa TFF Yawarudisha Waamuzi Wote Darasani

Thu, 10 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), jana Jumatano liliweka wazi kuwa limeandaa semina ya siku tatu kwa waamuzi wote wa Ligi Kuu Bara kwa ajili ya kuwaandaa na michezo ya mzunguko wa pili wa ligi hiyo.

Lengo kuu la semina hiyo ni kutazama, kupitia changamoto na kuboresha maeneo mbalimbali ili kuondoa zile sintofahamu za uamuzi Hii inakuja ikiwa ni siku chache baada ya kuwepo kwa malalamiko ya wadau mbalimbali wa soka juu ya changamoto za waamuzi kushindwa kuzitafsiri vema sheria za soka katika baadhi ya mechi za Ligi Kuu Bara zilizopita.

Katika malalamiko hayo, vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara, Yanga walienda mbali zaidi na kuandaa mkutano wa waandishi wa habari juzi Jumanne kuelezea masikitiko yao na mwenendo wa baadhi ya waamuzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live