Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF, Wadau watuma salamu za rambirambi,Pole kwa Mashabiki Namungo

TFF X NAMUNGO TFF, Wadau watuma salamu za rambirambi,Pole kwa Mashabiki Namungo

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa salamu za rambirambi kwa timu ya Namungo kufuatia vifo vya mashabiki wake wanne vilivyotokana na ajali ya gari iliyotokea eneo la Miteja mkoani Lindi.

"Rais Karia kwa niaba ya TFF ametoa pole kwa timu ya Namungo, familia, ndugu, jamaaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huo"

"Aidha amewaombea majeruhi kupona haraka na kurudi katika majukumu ya kila siku"

Bodi ya Ligi Kuu pia imesema imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali ya gari iliyokuwa ikisafirisha mashabiki wa klabu ya Namungo ya mkoani Lindi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametoa pole kwa familia za marehemu, wapenzi wa mpira na wote walioguswa na vifo vya mashabiki waliopatwa na ajali hii. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahaal pema na tunawaombea majeruhi wapone haraka

Klabu pia zimeendelea kutuma salamu za rambirambi ikiwemo KMC iliyotoa taarifa ikisema “Klabu ya KMC inaungana na Klabu ya Namungo FC pamoja na wanaruangwa wote katika kipindi hiki kigumu lakini pia tunawaombea majeruhi wote wapate nafuu mapema warejee katika majukumu yao"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live