Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF, RT yawapongeza viongozi wapya Taswa

Taswa Uchaguzi.jpeg TFF, RT yawapongeza viongozi wapya Taswa

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na lile la Riadha (RT), vimeupongeza uongozi mpya wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), na kuwatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.

TASWA ilifanya uchaguzi wake mkuu Jumapili, Februari 5 jijini Dar es Salaam, na Amir Mhando kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti, Wakili msomi, Alfred Lucas kushinda nafasi ya Katibu Mkuu.

Mwandishi wa Mwananchi, Imani Makongoro aliyepata kura zote za ndiyo alichaguliwa kuwa Katibu mkuu msaidizi, Dina Ismail Mweka Hazina na wajumbe ni Timzo Kalugira na Nasongelya Kilyinga.

TFF na RT kwa nyakati tofauti zimeupongeza uongozi mpya na kuahidi ushirikiano.

Taarifa ya rais wa TFF iliyotolewa na ofisa habari, Cliford Ndimbo imesema TFF itashirikiana na uongozi huo katika maendeleo ya mpira wa miguu kwenye eneo la kuhabarisha Umma.

"Waandishi wa habari ni moja ya nguzo muhimu, nampongeza Amir kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti na viongozi wengine wote," imeeleza taarifa ya Karia.

RT pia imetoa pongezi kupitia kwa msemaji wake, Lwiza John.

Amesema RT inatambua mchango mkubwa wa sekta ya habari katika maendeleo ya mchezo huo, hivyo wanawahakikishia ushirikiano wa kutosha.

"Tumepokea kwa faraja matokeo ya uchaguzi wa TASWA, na tunawapongeza viongozi wapya huku tukitarajia ushirikiano wa kutosha katika kuhamasisha maendeleo ya Riadha Tanzania, kitaifa na kimataifa," alisema Lwiza na kuongeza.

RT milango ipo wazi kwa TASWA na wanachama wake, hivyo wasisite kuwasiliana katika masuala mbalimbali yahusuyo mchezo wa riadha.

Chanzo: Mwanaspoti