Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa likiwa ndio mamlaka inayosimamia na kutoa vibali vya michezo ya soka nchini halijatoa kibali kwa ajili ya mashindano ya Ndondo Cup ambayo yametangazwa na Clouds Media.
Mashindano hayo yametangazwa rasmi leo Machi 22, 2023 na Mkurugenzi wa Mshindano hayo, Shaffih Kajuna maarufu kama Shaffih Dauda ambaye pia ni mtangazaji wa chombo hicho cha habari kupitia kipindi cha Clouds 360.
Hadi sasa imesema imetoa kibali kwa taasisi moja tu kuandaa mashindano ambayo yatafanyika katika kipindi cha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Ikumbukwe pia kuwa, Shaffih alifungiwa na Shirikisho hilo kujihusisha na masuala ya soka kwa miaka mitano.