Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF: Dirisha Dogo la usajili lipo wazi

Dirisha Dogo TFF: Dirisha Dogo la usajili lipo wazi

Fri, 16 Dec 2022 Chanzo: Dar24

Rasmi Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) limetangaza kufunguliwa kwa Dirisha Dogo la Usajili kwa Klabu za Ligi Kuu ya NBC, Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite.

TFF imethibitisha leo Desemba 16, 2022 kuwa siku maalum ya kufunguliwa kwa Dirisha hilo na Rasmi litafungwa Januari 15, 2023.

TFF imezitaka Klabu za Ligi Kuu ya NBC, Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite kutumia kipindi hiki kufanya usajili na kukamilisha uhamisho.

Hata hivyo Shirikisho hilo limesisitiza kuwa, wakati wote wa usajili Klabu itakayokutana na changamoto yoyote inapaswa kuwasiliana na Idara ya Mashindano TFF.

TFF imebainisha kuwa Baada ya kufungwa kwa Dirisha hakutakuwa na muda wa ziada na imeziagiza Klabu kukamilisha Usajili na uhamisho kwa wakati.

Chanzo: Dar24