Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESIZA SOKA: Timo Werner kuibukia Real Madrid

Timo Werner Timo Werner

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Liverpool, Manchester City na Brighton wapo kwenye rada ya kunasa saini ya beki Valentin Barco kutoka Boca Juniors.

Arsenal wanaripotiwa kulazimika kubadilisha mipango yao ya uhamisho katika dirisha dogo la uhamisho kwa kiungo wa klabu ya Fluminense Adre kwa sababu hapo hawaongozi tena kwenye mbio za kumsajili.

Raphael Varane anaweza kuwa chaguo la Bayern Munich katika dirisha dogo la uhamisho la mwenzi January.

Kizingiti pekee ni mshahara mkubwa ambao anapata United, ambapo, anadaiwa kupata pound million £17m kwa mwaka.

Klabu ya PSG-Paris Saint-German inalenga kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Napoli Khvicha Kvaratskheli ikiwa Kylian Mbappe ataondoka klabuni msimu wa joto.

Mazungumzo kati ya Khvicha Kvaratskheli na Napoli juu ya nyongeza ya mkataba yatafanyika pindi Hali ya ndani ya klabu hiyo itakapopata ufunguzi.

Real Madrid na Barcelona wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich Leroy Sane.

Tottenham inania ya kutaka kumsajili winga wa Barcelona Raphinha kwenye dirisha la January,

Real Madrid wanafikiria juu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji Timo Werner kwa mkopo katika dirisha dogo la uhamisho kama mbadala wa Vinicius Jr ambaye ameoata majeraha ya mda mrefu.

Timo Werner amekuwa sio chaguo la kwanza kwa RB Leipzig msimu huu.

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Anthony Martial anaweza kuondoka klabuni hapo ikiwa kuna ofa nzuri itapelekwa msimu huu wa baridi.

Chelsea wanafikiria kuwekeza pesa nyingi kwa mshambuliaji wa klabu ya Brentford Ivan Toney katika dirisha dogo la uhamisho la mwenzi January 2024.

Arsenal na Manchester United ni miongoni mwa vilabu vinavyotarajiwa kuonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa Brazil Marcos Leonardo, 20, ambaye wakala wake anasema atataka kuondoka Santos Januari.

Chelsea, Manchester City, Manchester United na Newcastle United zote zilituma wawakilishi kumtazama winga wa Napoli mwenye umri wa miaka 22 Khvicha Kvaratskhelia wakati wa kipigo cha 3-1 kutoka kwa Uhispania Jumapili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live