Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA USAJILI: Waarabu wamtupia jicho De Bruyne

KDB DD TETESI ZA USAJILI: Waarabu wamtupia jicho De Bruyne

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

FC Barcelona wanafikiria kuhamia kwa kiungo wa klabu ya Leicester City Wilfred Ndidi ambaye mkataba wake unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu

Klabu ya Getafe inapanga kupeleka ofa ya kumsajili mshambuliaji Mason Greenwood kutoka Manchester United kwa mkataba wa kudumu.

Wakati huo United wanaripotiwa kuwa wanapendelea kumtoa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa mkopo msimu mwingine zaidi.

Majogoo wa jiji Liverpool wanajindaa kwenda katika dirisha kubwa la uhamisho la msimu ujao kupata saini ya kiungo wa kati wa klabu ya Leeds United Archie Gray, ambaye anaweza kugharimu zaidi ya pound million £40m.

Chelsea wanapanga kufanya mazungumzo na klabu ya Nottingham Forest juu ya hatma ya kiungo wa kati mwenye umri wa miaka 19 Andrey Santos, ambaye amecheza mechi mbili tu toka amejiunga na klabu hiyo kwa mkopo.

Kiungo wa klabu ya Manchester City Kalvin Phillips anaelekea kujiunga na klabu ya Newcastle United kwa mkopo katika dirisha dogo la usajili hapo January badala ya Juventus.

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund Julian Brandt yupo kwenye rada za Newcastle United na Arsenal

Klabu ya Girona inataka kumsajili tena kiungo Oriol Romeu mwenye umri wa miaka 32 kutoka Barcelona.

Manchester United wanaweza kumteua Mkurugezi wa ufundi WA klabu ya Crystal Palace Dougie Freedman kama sehemu ya mapinduzi ya klabu chini ya mmiliki Jim Ratcliffe.

Kocha wa klabu ya Chelsea Mauricio Pochettino hatakuwa na ushawishi katika shughuli ya uhamisho wa klabu hiyo mwenzi January.

Klabu ya Al-Nassr imewasiliana na wawakilishi wa Kevin de Bruyne na wangependa kukutana na mchezaji huyo.

Lengo lao ni kueleza mradi wao wa mda ywa klabu ili kujaribu kumshawishi kuungana nao.

Arsenal walitaka kumuuza Thomas Partey mwenzi January, lakini jeraha lake la paja linamaanisha anaweza kubaki klabuni hapo zaidi ya dirisha la msimu huu wa baridi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live