Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA USAJILI: Varane kumkuta ya Jadon Sancho Man United

Raphael Varane Erik Ten Hag Manchester United Raphael Varane with Erik Ten Hag

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Arsenal wanatazamia kumnunua mshambuliaji wa Sporting Lisbon Viktor Gyokeres kama mbadala wa Ivan Toney.

Raphael Varane anaweza kuondoka Manchester United mwezi Januari baada ya kutofautiana na meneja Erik ten Hag.

Crystal Palace wanamweka beki wa kati wa Valencia, Cristhian Mosquera kwenye orodha yao fupi katika dirisha uhamisho kama mbadala Marc Guehi anahusishwa na Man United na Chelsea.

Everton wako tayari kumuuza beki wa kati wa England Ben Godfrey, 25, kwa Tottenham mwezi Januari iwapo dau litawasilishwa.

Manchester United wametoa ofa yenye mshahara mnono kwa beki wa Barcelona Ronald Araujo, 24, ambaye hana nia ya kuhamia Bayern Munich Januari.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Mathys Tel, 18, ameamua kusalia Bayern Munich angalau hadi msimu ujao wa joto, licha ya vilabu vingi kuuliza kuhusu uwezekano wa kupatikana kwa mkopo, ikiwa ni pamoja na Manchester United.

Chelsea wamefanya mazungumzo na Palmeiras kuhusu dili la kumsajili winga wa Brazil Estevao Willian, 16, anayejulikana kama 'Messinho', ambaye pia amewavutia Barcelona.

Kocha Mikel Arteta amemwalika gwiji wa Arsenal Dennis Bergkamp kurejea katika klabu kama sehemu ya wakufunzi wa akademi yao.

Fulham wanaongeza hamu yao ya kumnunua Msenegali wa Le Havre Arouna Sangante, 21.

Fulham pia wameonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Fluminense wa Brazil Andre, 22.

Liverpool ni miongoni mwa vilabu vya Premier League vinavyomtaka fowadi wa Kijerumani Maximilian Beier, 21, ambaye anatarajiwa kuondoka Hoffenheim msimu ujao wa joto.

Jamal Musiala alipoulizwa kuhusu Old Trafford:

"Ni ndoto ya watoto wengi kucheza hapo, Nilipokuwa mdogo siku zote nilifurahia kutazama michezo Old Trafford".

"Nadhani hali itakuwa nzuri. Man United watacheza kesho na bila shaka wana uboraā€¯

Liverpool wanavutiwa na kumpata mshambuliaji wa kati wa klab ya Hoffenheim Maximilian Beier, ambaye ana mabao 6 na asisti 4 kwenye Bundesliga hadi sasa msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live