Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA USAJILI: Rashford aigomea Spurs, kupigania namba United

Marcus Rashford Marcus Marcus Rashford

Fri, 10 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford ameigomea ofa ya Tottenham Spurs na badala yake anataka kuanza upya kuipambania namba ndani ya United.

Nyota huyo anataka kuanza kupambana upya msimu ujao chini ya Kocha Mkuu, Eric Ten Hag kwa mujibu wa taarifa.

Rashford mwenye miaka 24 alikuwa na msimu mbaya ndani ya Old Trafford kwa kuwa ametupia mabao manne na pasi mbili ndani ya Ligi Kuu England msim huu wa 2021/22.

Spurs ilikuwa inatajwa kuhitaji saini yake ili aweze kujiunga na kikosi chao na mkataba wake umebakiza mwaka mmoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live