Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA USAJILI: Pochettino akaa mkao wa kula Real Madrid

Mauricio Pochettino 4842395 Mauricio Pochettino

Thu, 23 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Arsenal, Chelsea na Manchester City wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Italia Wilfried Gnonto, 19, kutoka Leeds United.

Chanzo: [Gazzetta dello Sport, Via Metro]

Juventus na Napoli ni miongoni mwa vilabu kadhaa vya Italia ambavyo pia vinavutiwa na Gnonto.

Chanzo: [90min]

Manchester United inaweza kutumia mbinu mbadara kwa Tottenham kumnunua mlinda mlango Mwingereza Dean Henderson, 26, kuwashawishi Spurs kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 29.

Chanzo: [ESPN]

Mshambulizi wa Eintracht Frankfurt wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 24, ambaye analengwa kwa pauni milioni 105 na Manchester United, amependekeza kuwa yuko tayari kuhama msimu huu.

Chanzo: [L'Equipe, Via Mail]

Manchester City wamefufua nia yao ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Florian Wirtz, 19.

Chanzo: [90min]

Tottenham iko kwenye hatari ya kumkosa meneja wa zamani Mauricio Pochettino msimu wa joto huku Muajentina huyo akiwa juu kwenye orodha ya wanaotamani Real Madrid iwapo kocha wa sasa Carlo Ancelotti ataondoka.

Chanzo: [The Times]

Chelsea wamekubali kwamba watahitaji kupata hasara kubwa ikiwa wanataka kumuuza mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 29, msimu wa joto.

Chanzo: [Football Insider]

Matumaini ya Arsenal na Barcelona kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Martin Zubimendi kutoka Real Sociedad yanaonekana kuisha baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kusema hatarajii kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Chanzo: [Daily Mail Sport]

Barcelona wana nia ya kumsajili beki wa Monaco mwenye umri wa miaka 21 Vanderson.

Chanzo: [Sport – In Hispanic]

Vilabu kadhaa vimeonyesha nia ya kutaka kumsajili beki wa kushoto Mwingereza Brandon Williams, 22, kutoka Manchester United.

Chanzo: [Football Insider]

Kiungo wa kati wa Juventus na Ufaransa Adrien Rabiot, 27, amedokeza kuwa huenda akavutiwa na uhamisho wa kuelekea Liverpool.

Chanzo: [The Sun]

Chanzo: www.tanzaniaweb.live