Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA USAJILI: Liverpool wapiga hatua kubwa usajili wa Alexis Mac Allister

IMG 4122.jpeg Alexis Mac Allister

Sun, 21 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Liverpool wanakaribia kufikia kabisa makubaliano kuhusu masharti ya mkataba na kiungo wa kati wa Brighton, Alexis Mac Allister, 24, ingawa bado hawajasaini mkataba.

Source: [Fabrizio Romano]

Meneja wa Brighton Roberto de Zerbi ameiambia bodi ya klabu hiyo izuie kila dau kwa ajili ya winga Mjapan Kaoru Mitoma, 26, huku Mac Allister na kiungo wa kati wa Equador mwenye umri wa miaka 21- Moises Caicedo wakiwa tayari wamejiandaa kuondoka Seagulls msimu huu.

Source: [Football Insider]

Vilabu vitatu Arsenal, Liverpool na Barcelona zina nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Bayern Munich na Ujerumani, Joshua Kimmich, 28.

Source: [Marca - in Spanish]

Manchester City watatoa ofa ya kiungo wa kati wa Ujerumani Ilkay Gundogan, 32, ya mkataba mpya hadi mwezi Juni 2024 , mkataba ambao utakuwa na chaguo kwa ajili ya msimu zaidi, huku Barcelona wakiwa na nia naye.

Source: [Fabrizio Romano]

Meneja wa West Ham David Moyes anapanga kuondoka kaika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Source: [Football Insider]

Kiungo wa safu ya nyuma Manchester City na Ureno, Joao Cancelo anafuatiliwa kwa karibu na Barcelona, huku Bayern Munich wakiwa hawana uwezekano kabisa wa kurefusha zaidi mkataba wa mkopo na kijana huyo mwenye umri wa miaka 28.

Source: [Mundo Deportivo - in Spanish]

Hatahivyo, City wanafikiria kufanya mkataba wa kubadilishana wachezaji na Bayern Munich kwa ajili ya Kimmich ambao utairuhusu klabu hiyo kubwa katika Bundesliga giants kuendelea kuwa na Cancelo.

Source: [Mirror Sport]

Newcastle United wako mbele katika kinyang’anyiro cha kusaini mkataba na mlinzi wa Arsenal na Uskochi Kieran Tierney, 25, msimu huu, huku Manchester City na Aston Villa pia wakimtaka .

Source: [Football Insider]

Chelsea inataka kumhamisha msimu huu mlindalango wa Brentford na Uhispania David Raya, 27,ambaye anathamanishwa kwa karibu pauni milioni 40.

Source: [Givemesport]

West Ham wako tayari kumuacha mshambuliaji Muitalia Gianluca Scamacca arejee katika Serie A mwaka mmoja tu baada ya kujiunga na Sassuolo, huku AC Milan wakimfuatilia kwa karibu kijana huyo mwenye umri wa miaka 24.

Source: [Gazzetta dello Sport - in Italian]

Chanzo: www.tanzaniaweb.live