Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA USAJILI: Liverpool wanataka Bilion 124 usajili wa Mane

MANE.jpeg Sadio Mane

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Liverpool ya England imekataa ofa ya pili ya Bayern Munich ya kutaka kumsajili mshambuliaji Sadio Mane. Bayern wanamtaka Mane kama mbadala wa mshambuliaji Robert Lewandowski aliyeomba kuondoka katika klabu hiyo.

Awali Bayern Munich waliripotiwa kupeleka Ofa ya pesa za Ulaya Euro Milion 30 ambayo ni zaidi ya Bilioni 74 kwa pesa za Tanzania (74,982,670,404.81) kama ada ya uhamisho ya mchezaji huyo, mabingwa hao wa Ujerumani wakaboresha tena ofa yao kwa kupeleka tena dau la Euro milioni 35 ambayo ni sawa na Bilioni 87,473,097,250.55 kwa pesa za Tanzania lakini Liverpool wameikataa ofa hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti Liverpool wanataka dau la Euro million 50 kama ada ya uhamisho ya mshambuliaji huyo raia wa Senegal mwenye umri wa miaka 30 sawa na billioni 124,929,743,464.63 kwa pesa za Tanzania.

Mkataba wa Mane ndani ya kikosi cha Liverpool unamalizika mwezi Juni mwaka 2023, na mshambuliaji huyo mara kadhaa ameonyesha nia yakutaka kuondoka katika klabu hiyo.

Bayern wanamuwania Mane kama mbadala wa Robert Lewandowski ambae ameomba kuondoka akihusishwa kujiunga na FC Barcelona ya Hispania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live