Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA USAJILI: Liverpool waingia mazima kwa Jamal Musiala

Jamal Musiala Kinda wa Bayern Munich, Jamal Musiala

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Liverpool wanafikiria kusonga mbele kwa Jamal Musiala ambaye hafurahishwi na muda wake wa kucheza anaopata ndani ya kikosi cha Bayern Munich chini ya Thomas Tuchel.

Real Madrid wapo tayari kufanya biashara na Chelsea juu ya mkataba wa kudumu wa Kepa Arrizabalaga, lakini hawatalipa ada ya zaidi ya pound million £17.5 kwa kipa huyo ambaye aligharimu Chelsea takribani pound million £71.6 miaka 5 iliyopita.

Juventus inaweza kutumia mshahara ambao umeokolewa kwa Paul Pogba kumsajili Thomas Partey katika dirisha la uhamisho la mwenzi January kwa mkopo.

Pogba anakabiliwa na kizuizi cha mda mrefu cha kutojihusisha mpira wa miguu, hali ambayo itafanya kupunguza kwa mshahara wake kutoka Juventus.

Chelsea wameonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Bayer Leverkusen Florian Wirtz (20) pia anawindwa na Manchester City.

Kocha wa klabu ya Chelsea Mauricio Pochettino anavutiwa na kipa wa klabu ya Athletic Bilbao Unai Simon.

Maafisa wa Saudi Pro League wanamtaka kiungo wa klabu ya Manchester City Kevin de Bruyne, ambaye anaweza kugharimu takribani pound million £50m, ili kujiunga na ligi hiyo.

Kocha wa arsenal Mikel Arteta amewaongeza Martin Zubimendi na Aurelien Tchouameni kwenye orodha malengo yake katika dirisha la uhamisho.

Liverpool hawana mpango wa kumuuza Mohamed Salah mwenzi January, bila kujali ofa yoyote kutoka katika vilabu vya Saudi Pro League.

Mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Manchester United na beki wake Aaron Wan-Bissaka yanaonekana kukwama, na klabu hiyo italenga kuongeza mwaka 1 katika mkataba wake wa sasa.

Klabu ya Brentford ipo tayari kumuuza mshambuliaji wake Ivan Toney kwa dau la pound million £80m katika dirisha dogo la usajili la January 2024.

Chelsea, Tottenham na Arsenal wanahusishwa kutaka saini ya mshambuliaji huyo.

Borussia Dortmund wako tayari kumruhusu Jamie Bynoe-Gittens kuondoka klabuni hapo kwa mkopo January huku wakiendelea kuchunguza urejeo wa Jadon Sancho klabuni hapo.

Kipa wa Manchester United Andre Onana amekubali kuitumikia timu yake ya taifa ya Cameroon kwenye michuano ya AFCON mwenzi January 2024 na anaweza kukosa mechi takribani 7 za ndani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live