Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA USAJILI: Kichuya anukia Azam

KICHUYA.png Shiza Kichuya

Sun, 3 Jul 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Tajiri wa jiji la Dar es Salaam, Yusuf Bakhresa ameamua hivyo ndio unaweza kusema baada ya kuendelea kushusha vifaa ndani ya timu hiyo tayari kwa msimu wa 2022/23 na michuano ya kimataifa.

Azam FC leo Jumapili (Julai 3) inatarajia kumtangaza winga Shiza Kichuya kutoka Namungo FC kwa mujibu wa chanzo cha ndani kutoka ndani ya klabu hiyo ambayo imepanga kumtambulisha staa huyo saa 12 jioni.

Hadi sasa tayari wamesajili mastaa wanne wawili wa kigeni na mmoja mzawa ambao ni Cleophace Mkandala na Isah Ndala wote viungo, Kipre Junior na Tape Edinho.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz