Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA USAJILI: Kane aziingiza vitani Bayern, Man United

HARRY KANE M 1140x640 Harry Kane

Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bayern Munich wanavutiwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa England na Tottenham Hotspur Harry Kane, 29, inaelezwa kuwa United wameonyesha nia ya kumsajili pia.

Liverpool, Chelsea na Manchester United wanakusudia kumshawishi kiungo wa Brighton Hove Albino Alexis Mac Allister, 24, ambaye anaweza kuondoka kipindi cha kiangazi.

Real Madrid wako tayari kutuma ofa nzuri ya kumhitaji beki wa kulia wa Chelsea na England Reece James, 23 ambapo kiangazi klabu hiyo italazimika kuuza baadhi ya wachezaji ili kuleta uwiano kifedha.

Aliyekuwa kocha wa Bayern Munich Julian Nagelsmann, 35, amekaribishwa kufika kwenye bodi ya Chelsea ambayo inaendelea kusaka kocha mpya, kocha wa zamani wa Hispania Luis Enrique, 52, alishakutana na bodi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live