Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA USAJILI: Joao Palhinha ageuka lulu Ulaya

Arsenal Na Chelsea Kwenye Mbio Kumsaka Nyota Wa Fulham Joao Palhinha Joao Palhinha

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Real Madrid wamefikia makubaliano ya kumsajili beki wa kushoto wa Bayern Munich na Canada Alphonso Davies, 23, na watatarajia kukamilisha dili hilo msimu huu wa joto au mwakani mwezi June 2025, atakapokuwa mchezaji huru.

Mustakabali wa Meneja wa chelsea Mauricio Pochettino haujulikani baada ya timu yake kupoteza mchezo wa Fainal ya Kombe la Carabao dhidi ya Liverpool, huku kocha wa Sporting Lisbon Ruben Amorim akitarajiwa kuchukua mahala pake.

Manchester United inatarajiwa kuwatoa wachezaji kadhaa msimu huu wa joto huku winga wa Brazil Antony, 24, akiwa miongoni mwa wale ambao watakuwa tayari kuwauza.

Chelsea wanatumai kuwauza beki Trevoh Chalobah, 24, na fowadi wa Albania Armando Broja, huku mustakabali wa kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 24, na beki wa kushoto wa Uhispania Marc Cucurella, 25, ukiwa shakani huku wakitarajia kufanya mabadiliko makubwa msimu huu wa joto.

Bayern Munich, Liverpool na Arsenal wako kwenye mbio za kumnunua kiungo wa kati wa Fulham na Ureno Joao Palhinha, 28, msimu wa joto.

Kiungo wa kati wa Manchester City Kevin de Bruyne angependelea kuhamia Major League Soccer (MLS) badala ya Saudi Pro League.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anatimiza miaka 33 msimu huu wa joto, wakati mkataba wake unaingia mwaka wake wa mwisho.

Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane, 51, yuko tayari kufundisha nchini Italia, huku nyota huyo wa Ufaransa akihusishwa na kurejea kwenye klabu ya Juventus akiwa kama Meneja mpya.

Kipa wa uingereza Aaron Ramsdale, 25, anatamani kuondoka Arsenal msimu wa joto baada ya kupoteza nafasi yake kwa kipa wa Uhispania David Raya, 28.

Tottenham Hotspur wanaongoza katika mbio za kutaka kumnunua mchezaji wa Hull City Jaden Philogene, 22, ingawa Aston Villa wana kipengele cha kumnunua winga huyo wa chini ya miaka 21 wa Uingereza.

Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Omari Forson,19, anaweza kuondoka Manchester United msimu huu wa joto, huku kandarasi wa kiungo huyo mshambuliaji ikimalizika mwezi June huko Old Trafford.

Celtic wanatazamia kumnunua mlinda mlango wa Liverpool na Jamhuri ya Ireland Caoimhin Kelleher, 25, huku wakitafuta Golikipa nambari moja kwa msimu ujao.

Nice na beki wa kati wa Ufaransa Jean-Clair Todibo, 24, ana nia ya kurejea Barcelona licha ya kutakiwa na Manchester United.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live