Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA USAJILI: Golikipa aikataa Man United

Zion Suzuki Japan 752x428 Goalkeeper wa kimataifa wa Japan Zion Suzuki

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya AFC Leopard ya nchini Kenya imemteua Tom Juma kuwa kocha wao mkuu pamoja na Fred Ambani kuwa kocha wao msaidizi.

David De Gea ni moja ya jina linalotajwa kwa siku za hivi karibuni katika orodha ya makipa ya Bayern Munich.

Mabingwa wa ligi ya Ujerumani wanataka kuanza mawasiliano ili kuona kama wanaweza kunasa saini kipa huyo wa kimataifa wa Hispania ambaye kwa sasa ni free Agent baada ya mkataba wake kumalizika huko Manchester United.

Klabu ya Fulham imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Mexico Raul Jimenez kutoka Wolverhampton Wanderers kwa ada ya pound million £5.5m kwa mkataba wa miaka 2 plus mwaka 1 wa ziada.

Goalkeeper wa kimataifa wa Japan Zion Suzuki amekataa ofa ya kwenda kujiunga na klabu ya Manchester United.

Manchester United itatoa ofa rasmi wiki hii kwenda Atalanta kwa ajili ya kupata saini ya mshambuliaji Rasmus Højlund, lakini hawatalipa zaidi.

United tayari wamekubaliana na Højlund kwa mkataba wa miaka 5 na mwaka mmoja zaidi wa hiari.

Klabu ya TP Mazembe imekamilisha usajili wa goalkeeper Alioune Badara Faty (24) kwa mkataba wa miaka 2 kutoka Casa Sport ya Senegal.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live