Mchezaji wa Kimataifa wa Uholanzi Matthijs De Light amethibitisha kuwa yupo kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba na klabu ya Juventus, japokuwa hakuna makubaliano waliyoafikiana mpaka sasa.
De Light mkataba wake na vibibi vya Turin unaisha June 2024, kuna taarifa nchini Italia zinasema mlinzi huyo yuko tayari kusaini kuongeza mwaka mmoja mbele kwenye mkataba wake, ikiwa ada ya kuvunja mkataba itapunguzwa kutoka ya sasa €125 milion hadi kufikia €70 milioni.
“Bado tupo kwenye mazungumzo, lakini sio sababu kwamba ndio tayari tuna makubaliano, kama ilivyoandikwa.” De Light alisema.
“Sio kweli. Makubaliano bado yanaendelea lakini bado yapo kwenye hatua za mwanzo. Bado nina miaka miwili kwenye mkataba wangu, kwaiyo bado nina muda wa kutosha kabisa”
De Ligt alijiunga na klabu ya Juventus akitokea Ajax kwa uhamisho wenye thamani €85m kwenye majira ya kiangazi mwaka 2019. Mkataba wake na Bianconeri unaisha mwaka June 2024.