Chelsea wameingia katika mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, msimu huu. Hitaji hilo linatoa picha ya hatari kwa Mshambuliaji wao Rumelu Lukaku aliyepo kwa mkopo Inter Milan.
Chanzo: [Evening Standard]
Chelsea pia wanajipanga kuwasilisha ombi la kumnunua beki wa kushoto wa Barcelona na Hispania Alejandro Balde, 19, ili kuchukua nafasi ya beki wao wa England Ben Chilwell, 26.
Chanzo: [The Sport]
Bayern Munich wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Kai Havertz, 23, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani akionyesha nia ya kuungana tena na meneja wake wa zamani Thomas Tuchel.
Chanzo: [90min]
Paris St-Germain wamemwambia Lionel Messi kwamba watalipa chochote kinachohitajika ili kumbakisha mshambuliaji huyo wa Argentina, 35, huku kukiwa na ripoti kwamba Barcelona wamewasiliana na Messi kuhusu uwezekano wa kurejea Camp New.
Chanzo: [Mundo Deportivo]
Arsenal wanamtaka kiungo wa kati wa Real Madrid Aurelien Tchouameni ili kuboresha kikosi chao msimu wa joto, huku Liverpool pia ikidaiwa kumtaka Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 23.
Chanzo: [El Nacional]
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alisema klabu hiyo imekuwa na shughuli nyingi wakati wa mapumziko ya kimataifa ikipanga malengo ya msimu wa joto na iko tayari kutumia pesa nyingi katika soko la usajili majira ya joto.
Chanzo: [The Mirror Sport]
Mshambulizi wa Chelsea Pierre-Emerick Aubameyang, 33, anataka kurejea Barcelona lakini The Blues hawataki kumuuza moja kwa moja mshambuliaji huyo wa Gabon.
Chanzo: [The Sport]
AS Roma wanafikiria kumnunua mlinda mlango wa Manchester United David de Gea, huku Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 32 mkataba wake utakapotamatika msimu wa joto huko Old Trafford.
Chanzo: [Fichajes]
Wachezaji wawili wa Crystal Palace na Ghana Jeffrey Schlupp, 30, na Jordan Ayew, 31, wametia saini kandarasi mpya huko Eagles.
Chanzo: [The Athletic]