Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA USAJILI: Bosi Man United aanza na usajili huu

Joao Neves Joao Neves

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mmiliki mpya wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe anatazamiwa kuidhinisha dau la zaidi ya £100m kwa kiungo wa kati wa Benfica Mreno Joao Neves, 19.

Manchester United itafanya kila iwezalo kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich na Uingereza Harry Kane, 30, iwapo atapatikana msimu huu wa joto.

Liverpool wamemchagua meneja wa Brighton Roberto de Zerbi, bosi wa Ujerumani Julian Nagelsmann na Ruben Amorim wa Sporting Lisbon kama wagombea wakuu wa kuchukua nafasi ya Jürgen Klopp.

Kiungo wa kati wa Ujerumani Joshua Kimmich, ambaye amekuwa akihusishwa na Manchester United, Manchester City na Liverpool, bado hajafanya mazungumzo ya kandarasi na Bayern Munich ikiwa imesalia chini ya miezi 18 katika mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29.

Arsenal wako tayari kumuuza beki wa pembeni Kieran Tierney msimu wa joto lakini The Gunners wanataka £20m kwa mlinzi huyo wa Scotland mwenye umri wa miaka 26.

Chelsea bado hawajafanya maamuzi kuhusu mustakabali wa kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 24, licha ya Tottenham kumtaka.

Chelsea inaweza kutarajia kuuza wachezaji 15 katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Manchester United inanuia kuongeza mshahara mara tatu wa kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 18, chini ya mwaka mmoja baada ya kusaini mkataba mpya, ili kumbakisha klabuni hapo hadi mwezi June 2030.

AC Milan wanasalia kwenye mazungumzo na Arsenal kuhusu uhamisho wa beki wa kushoto wa Poland Jakub Kiwior, 24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live