Miamba ya soka Bundesliga, Bayern Munich imepandisha dau la Pauni 30 milioni kwaajili ya kunasa saini ya fowadi wa Liverpool, Sadio Mane kwa mujibu wa ripoti.
Ofa ya kwanza ya Bayern Munich, Pauni 21 milioni ilipigwa chini na Liverpool, lakini sasa imejipanga upya na kuongeza dau kufika hadi Pauni 30 milioni.
Aidha Liverpool imegoma kumuuza kwa Mane bei chee, kutokana na thamani ya nyota huyo aliyekipiga Anfield kwa muda miaka sita.
Kwa mujibu wa ripoti Liverpool inataka ofa ya kitita cha Pauni 42.5 milioni, itakayotumika katika usajili wa Darwin Nunez, anayewindwa na Jurgen Klopp kama mbadala wa Mane.
Mane amebakiza mkataba wa mwaka mmoja kukipiga Liverpool, licha ya kuweka wazi hana mpango wa kuendelea kukipiga Anfield msimu ujao.