Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA USAJILI: Barcelona macho yote kwa Ngolo Kante

Ngolo Kante JPG Kiungo wa Chelsea, Ngolo Kante

Mon, 12 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Barcelona wanaweza kumaliza dili la kumsajili kiungo mkabaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa Ng’olo Kante 31, kama mchezaji huru wakati kandarasi ya mchezaji huyo itakapomalizika Stamford Bridge.

AC Milan huenda wakaishia njiani na matamanio ya kumsajili winga wa kimataifa wa Morocco na Chelsea Hakim Ziyech, 29, kutokana na mshahara mkubwa ambao mchezaji huyo anahitaji.

Tottenham wanaweza kumsajili beki wa Inter Milan na taifa la Uholanzi Stefan de Vrij, 30, katika dirisha dogo la usajili la Januari, hata hivyo wanaweza kukutana na upinzani wa Atletico Madrid.

Kocha wa Manchester United Erik ten Hag amesema alikuwa tayari kumuachia kwenda klabu nyingine aliyekuwa mshambuliaji wake staa Cristiano Ronaldo, 37, mwezi Agosti hata hivyo hakuna klabu iliyoonyesha nia ya kumsajili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live