Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA SOKA: Pochettino kuchukua nafasi ya Gerrard Aston Villa

Ochettino Mauricio Mauricio Pochettino

Tue, 18 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aston Villa wanavutiwa kumsajili kocha wa zamani wa Tottenham Hotspur na Paris St-Germain Mauricio Pochettino ambaye kwa sasa hana timu kwenda kuichukua nafasi ya Steven Gerrard.

Kocha wa Chelsea Graham Potter yuko kwenye matamanio ya kuungana tena na kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji na Brighton Leandro Trossard, 27, itakumbukwa wawili hao walikuwa pamoja Brighton Hove Albion kabla ya Potter kwenda Stamford Bridge.

Kiungo mkabaji wa Chelsea na Ufaransa N’Golo Kante hajafikia mwafaka wa kuongeza mkataba mpya na The Blues pamoja na mara kadhaa kuombwa aongeze kandarasi mpya.

Diego Simeone, kocha wa Atletico Madrid amesema hawezi kumsajili Cristiano Ronaldo 37, kwenye dirisha dogo la usajili la Januari kwa sasa mchezaji huyo bado anahusishwa kujiunga na Real Madrid.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live