Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA SOKA: Mbappe yuko njia panda PSG

Kylian Mbappe Gg Kylian Mbappe

Sat, 15 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Real Madrid kufikia sasa bado haijaamua kujaribu tena kumsajili mshambuliaji nyota wa Paris St-Germain Mfaransa Kylian Mbappe,23. Kwa sasa klabu hiyo kubwa ya Uhispania inamfuatilia kwa karibu kiungo wao wa zamani Xabi Alonso ambaye kwa sasa ni kocha wa Bayer Leverkusen wakiwa na nia ya kumchukua . (ESPN)

Mshambuliaji Kylian Mbappe anaangalia uwezekano wa kuvunja mkataba wake mwenyewe na kuondoka PSG mwezi Januari. (L'Equipe via Mail)

Klabu ya Inter Milan inataka kumsajili moja kwa moja mshambuliajji Romelo Lukaku mwishoni mwa msimu. Lukaku, 29, yupo Inter akitokea Chelsea kwa mkopo. (Calciomercato - in Italian)

Inter pia wanapiga hesabu za kumnasa beki wa kati wa Everton rai awa Colombia, Yerry Mina, 28. (Calciomercato - in Italian)

Manchester United wanapigiwa upatu kuwa vinara kusaini mkataba na mlindalango Mreno wa timu ya Porto mwenye umri wa miaka 23, Diogo Costa. (Diario de Noticias, via TeamTalk)

Wakati huo huo United wanatarajiwa kurefusha mkataba wa Diogo Dalot ili kuwazuia Barcelona ambao wanamuwinda mlinzi huyo Mreno mwenye umri wa miaka 23. (ESPN, via Mirror)

Newcastle United wanataka kukubali kusaini mkataba mpya mrefu na kiungo wa kati Mbrazil Bruno Guimaraes, 24, kabla ya kumalizika kwa msimu. (90min)

Arsenal watalazimika kulipa pesa zaidi ili kumnasa winga wa Ukraine Mykhaylo Mudryk, 21, katika dirisha la usajjili la mwezi Januari kama klabu yake ya Shakhtar Donestk itafanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya. (Football.London)

Tottenham inapanga kufungua mazungumzo ya mkataba na meneja Antonio Conte mwezi ujao. Mkataba wa sasa wa Muitaliano huyo mwenye umri wa miaka 53 unafifikia tamati mwishoni wa msimu huu. (Mail)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live