Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA SOKA: Martinelli aongeza Mkataba Arsenal

Gabriel Martinelli 1024x739 Martinelli arefusha Mkataba ndani ya Arsenal

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fowadi wa Brazil Gabriel Martinelli, 21, ameongeza mkataba mpya wa kuendelea kukitumikia kikosi cha Arsenal, kandarasi itakayofikia tamati majira ya kiangazi 2027.

Newcastle United imejitanua kwa kujiweka daraja moja na Real Madrid, Liverpool katika kumhitaji kiungo mkabaji wa England na Borussia Dortmund Jude Bellingham, 19.

Chelsea huenda ikalazimika kuwauza baadhi ya wachezaji wazawa endapo klabu hiyo itashindwa kufuzu kucheza Uefa msimu ujao kutokana na hofu ya panga la usawa wa matumizi katika uchumi (FFP).

Wakala wa Moises Caicedo, 21, amekosoa kitendo cha klabu ya Brighton kumzuia kiungo huyo kujiunga na Arsenal katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari, akisema kuwa fursa kama hiyo inaweza isitolee tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live