Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA SOKA: Man United kuvunja Mkataba wa Ronaldo?

Skysports Cristiano Ronaldo 5823297 Cristiano Ronaldo

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester United wanaweza kufikiria kuvunja mkataba wa fowadi wa Ureno Cristiano Ronaldo kufuatia mahojiano yake na Piers Morgan lakini watasubiri hadi watakaposikia mahojiano kamili kabla ya kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37.

Ronaldo anaweza kwenda Chelsea baada ya fowadi huyo kuhusishwa na kuhamia Stamford Bridge majira ya joto lakini iliripotiwa kuzuiwa na meneja wa wakati huo Thomas Tuchel.

Manchester United wameungana na Arsenal kumsaka winga wa Shakhtar Donetsk na Ukraine Mykhaylo Mudryk, huku mkufunzi wa United Erik ten Hag akisemekana kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 tangu alipokuwa meneja wa Ajax.

Mudryk alisema katika mahojiano na Vlada Sedan, mke wa beki wa Arsenal Oleksandr Zinchenko, kwenye chaneli yake ya YouTube kwamba "afadhali kuwa katika kikosi cha kwanza cha Arsenal kuliko kukaa kwenye benchi ya Real Madrid". Lakini winga huyo wa Ukraine, 21, anataka kuzungumza na meneja wa Gunners Mikel Arteta kabla ya kuamua kuhusu mustakabali wake.

Liverpool wanavutiwa na kiungo wa Las Palmas Alberto Moleiro, huku Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 19 pia anadaiwa kulengwa na Barcelona na Manchester City. (Express)

Roma inaweza kusikiliza ofa kwa mshambuliaji wa Uingereza Tammy Abraham, 25.

Tottenham ilituma maskauti kumtazama mshambuliaji wa Ufaransa Marcus Thuram, 25, kutoka Borussia Monchengladbach, na mshambuliaji wa Cameroon Youssoufa Moukoko, 19, wa Borussia Dortmund, kwenye mechi ya Ijumaa ya Bundesliga kati ya pande hizo mbili.

Liverpool na Arsenal pia wanamtaka Thuram wa Borussia Monchengladbach - Mfaransa huyo anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu na amekuwa akihusishwa pakubwa na Bayern Munich.

Chelsea wana imani kuwa wamefanikiwa kufikia makubaliano na mshambuliaji wa RB Leipzig Christopher Nkunku na kwamba Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 25 atajiunga Januari au msimu wa joto.

Manchester City wanapanga mazungumzo na wakala wa kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva wakati wa Kombe la Dunia ili kuamua mpango wa maisha yake ya baadaye. Mabingwa hao wa Premier League wanafahamu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anataka kujiunga na Barcelona na hatamzuia iwapo ofa sahihi itatolewa.

Beki wa kulia wa Leeds United Muingereza Cody Drameh, 20, anavutiwa na Newcastle United, pamoja na Lille, Borussia Dortmund na Bayer Leverkusen. (Fabrizio Romano)

Thomas Tuchel lazima aondoke Uingereza mwezi Disemba, kutokana na sheria za baada ya Brexit, baada ya kutimuliwa Chelsea, lakini makocha wake wawili, Zsolt Low na Benjamin Webber, ambao wamepewa likizo ya bustani, wanaweza kubaki kwa sababu bado wako chini ya mkataba wa kiufundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live