Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA SOKA: Man United kumpiga bei Casemiro

Casemiro 4 Games Casemiro

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester United watafikiria ofa kwa timu ambazo zimeonyesha Nia kwa kiungo wa kimataifa wa Brazil Casemiro, tayari vilabu vya Saudi Arabia vinalenga kupeleka ofa ya pesa kubwa kwa ajili ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31.

Chelsea hawataweza kutoa ofa kwa mshambuliaji wa Napoli Victor Osimhen katika dirisha dogo la uhamisho la mwenzi January.

Hata hivyo, inasemekana kuwa Osimhen yupo tayari kuhamia Stamford Bridge, lakini Chelsea watalazimika kusubili hadi msimu ujao wa joto.

Beki wa kati wa klabu ya Nice na timu ya taifa ya Ufaransa Jean-Clair Todibo, ameibuka kama kipaumbele cha kwanza kwa Manchester United katika dirisha dogo la uhamisho la January.

Manchester United na Tottenham Hotspur wanaungana na Liverpool na Arsenal katika mbio za kuwania saini kiungo wa kati wa klabu ya Fluminense Adre mwenye umri wa miaka 22.

Klabu ya Barcelona imeweka ada ya euro million €70= (£60.8) kwa klabu ambayo itahitaji kumsajili winga wake wa kimataifa wa Brazil Raphinha.

Kiungo wa kati wa klabu ya RB Leipzig na timu ya taifa ya Sweden Emil Forsberg amekubali kujiunga na klabu ya New York Red Bulls ya nchini Marekani mwenzi January.

Charlton na Leyton Orient wameonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji kinda Jamie Donley kutoka Tottenham Hotspur.

Kiungo wa klabu ya Arsenal Jorginho (31) amesema angependa kurejea kucheza soka katika vilabu vya nchini kwao Italia kabla ya kustaafu kucheza soka.

Juventus iliwasiliana na Manchester United juu ya uhamisho wa mkopo wa winga wa kimataifa wa Uingereza Jadon Sancho (23) wiki iliyopita.

Kiungo wa klabu ya Fulham FC na timu ya taifa ya Ureno João Palhinha amesema kukwama kwa uhamisho wake kwenda Bayern Munich katika siku ya mwisho umemuathili Sana.

Arsenal wameambiwa na Klab ya Al Hilal kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuipata saini ya Mreno Ruben Neves.

Inadaiwa kuwa Klabu ya Manchester United, wapo tayari kumuuza kwa bei ya hasara mchezaji wao Antony Santos, ikiwa ni miezi 18 tangu mchezaji huyo ajiunge kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 85, akitokea AFC Ajax mwaka 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live