Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA SOKA: Dani Alves kufungwa miaka 9

Dani Alves Pp Beki wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Dani Alves

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kushoto wa Chelsea Ian Maatsen, 21, yuko tayari kujiunga na Manchester City baada ya washindi hao watatu kuhusishwa na kutaka kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi chini ya miaka 21.

Chelsea pia inawafuatilia mshambuliaji wa Feyenoord na Mexico Santiago Gimenez, 22, na winga wa Real Betis kutoka Senegal Assane Diao, 18, kwa kutarajia dirisha la uhamisho la Januari.

Nyota wa Real Madrid Rodrygo amerejea kutoka Brazil akiwa na tatizo kwenye goti. Atafanyiwa vipimo leo kujua ukubwa wa Jeraha.

Bundi kawavamia Real Madrid majeruhi kila kukicha kumbuka wiki iliyopita wachezaji wao wawili walipata majeraha wakitumikia timu zao za taifa Eduardo Camavinga pamoja na Vinicius Junior.

Ángel Di Maria amethibitisha kuwa Copa América itakuwa michuano mara ya mwisho kuvaa jezi ya Argentina.

Manchester United, Arsenal na vilabu kadhaa vya Saudia vinavutiwa na winga wa Ureno Pedro Neto, 23, lakini Wolves watadai ada ya angalau £60m.

Chelsea wanamfuatilia winga wa Palmeiras Mbrazil Estevao Willian, 16, ambaye anasemekana kuwa na kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 52.

Barcelona imeonyesha nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham na Argentina Giovani Lo Celso, 27, huku wakitafuta hifadhi ya kiungo wa kati wa Uhispania Gavi, 19.

Raphaël Varane hajafurahishwa na hali iliyopo sasa Pale Manchester United na anataka kuondoka.

Manchester nited wanatarajia kupokea pesa kati ya €20M-€30M.

Mwendesha mashtaka wa umma huko Barcelona ameomba kifungo cha miaka 9 jela kwa Dani Alves (ambaye anatuhumiwa kumbaka msichana usiku).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live