Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI ZA SOKA: Ajitoa Timu ya Taifa kisa Rais kumpiga busu mchezaji

Cropped GettyImages 1438894334 Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Spain na Real Betis Borja Inglesias

Fri, 25 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Spain na Real Betis Borja Inglesias ametangaza rasmi kuwa hataichezea timu ya Taifa ya Spain hadi mambo yatakapobadilika,

Hii ni kutokana na kauli na kitendo cha Rais wa Shirikisho la Nchi hiyo ya Spain Luis Rubiales kumbusu Mwanadada Jenni Hermoso kisha kijigamba kuwa Mwanadada huyo ndio alilazimisha busu hilo na hakuna adhabu,

Mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku sasa ameamua kuachana na nia ya kujiunga na klabu ya Juventus kwa sababu wameshindwa kukubaliana,

Chelsea iko tayari kumruhusu Lukaku kujiunga na klabu yoyote ile ila kwa mkopo.

Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Spain Luis Rubiales amekataa kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu wazifa wake kwa tuhuma ya KUMBUSU Kwa Lazima Jenni Hermoso Hadharani,

Raia huyu amesema kuwa Jenni Hermoso yeye ndio alichochea Busu hilo, Luis Rubiales alisisitiza kwenye mkutano wa FA Spain kuwa Hatajiuzulu,

Alisema maana ya busu hilo ni kuheshimiana na kukubaliana na anasema kuwa ni heshima busu kuliko kupena mkono, Pia Rais huyo Alisema kuwa ni yeye ndio alimpa mkataba wa miaka (4) kocha wa Timu ya taifa ya Spain Jorge Vilda Hadharani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live