Fri, 17 Dec 2021
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Baada ya Sintofahamu inayoendelea ya muda sasa kati ya matajiri wa Jiji Azam FC, na nyota wake Mudathir Yahya, hatimae kuna taarifa zinazodai mchezaji huyo yuko mbioni kujiunga na Simba SC.
Mudathir na wenzake wawili walisimamishwa ndani ya klabu ya Azam kwa muda usiojulikana kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu.
Katika taarifa yake Azam FC, hawakuweka wazi hasa makosa hayo ni yapi waliyofanya wachezaji hao waandamizi ndani ya Klabu hiyo.
Wachezaji wengine waliosimamishwa ni Aggey Morris na Abubakar Salum "Sure Boy" ambae nae anazungumzwa kuhitajika Jangwani.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live