Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI: Lukaku njia panda hatma yake Chelsea, Inter Milan

Lukaku.jpeg Romelu Lukaku

Mon, 13 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku anataka kusalia Inter Milan mkopo wake utakapoisha, lakini klabu hiyo ya Italia haiwezi kumudu mshahara wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 hayumo katika mipango ya Graham Potter katika klabu ya Chelsea kwa sasa.

Chanzo: [Daily Mail Sport]

Paris St-Germain wameungana na Chelsea na Manchester United katika harakati za kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 24, kutoka Napoli.

Chanzo: [Nicolo Schira]

Chelsea na Newcastle wanafuatilia hali ya Raphinha huko Barcelona kwani klabu hiyo ya Uhispania inaweza kuwa tayari kumuuza winga huyo wa Brazil, 26.

Chanzo: [Sport - in Spanish]

Manchester United wanaangalia uwezekano wa kumnunua Joao Palhinha wa Fulham majira ya joto, ingawa Arsenal, Chelsea, Liverpool, Newcastle na Tottenham pia wanamfuatilia kiungo huyo wa Ureno, 27.

Chanzo: [The Sun]

Liverpool wanasemekana kuwa tayari kumchukua kiungo Joao Palhinha wa Fulham msimu huu wa joto.

Chanzo: [Daily Mail Sport]

Manchester City wanavutiwa na Ben Chilwell, 26, kwa kuwa beki huyo wa kushoto wa Uingereza anaweza kuwa sehemu ya "kuondolewa kwa wingi" huko Chelsea msimu huu wa joto.

Chanzo: [Athletic- registration is required]

Nottingham Forest haiko tayari kumpa mshambuliaji wa Uingereza Jesse Lingard, 30, mkataba mpya mkataba wake wa mwaka mmoja utakapokamilika msimu huu.

Chanzo: [Football Insider]

Inter Milan itajaribu tena kumsajili Victor Lindelof kutoka Manchester United msimu wa joto baada ya kushindwa kuafikiana kwa mkopo na beki huyo wa Sweden, 28, mwezi Januari.

Chanzo: [The Sun]

Inter Milan wanapigiwa upatu kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Marcus Thuram, 25, kutoka Borussia Monchengladbach, licha ya Juventus, Manchester United na Newcastle kuwinda saini yake.

Chanzo: [Calciomercato - in Italian]

Arsenal imekuwa ikimnyatia winga wa Ufaransa Moussa Diaby, 23, kwa miaka miwili iliyopita katika klabu ya Bayer Leverkusen lakini huenda pia Newcastle na Paris St-Germain zikawa na nia ya kutaka kuulizia msitakabali wake.

Chanzo: [Fabrizio Romano]

Vitor Roque amepinga uwezekano wa kuhamia Arsenal huku mshambuliaji huyo wa Brazil, 18, akipendelea kuhamia Barcelona kutoka Athletico Paranaense.

Chanzo: [Sport - in Spanish]

Atletico Madrid wamejitokeza kuwania saini ya mshambuliaji wa Brazil Roberto Firmino, 31, kama mchezaji huru wakati mkataba wake wa Liverpool utakapokamilika msimu huu wa joto.

Chanzo: [Mundo Deportivo - in Spanish]

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 29, anataka kusalia Juventus, licha ya kucheza mechi mbili pekee tangu ajiunge na klabu hiyo ya Italia kutoka Manchester United msimu uliopita wa joto.

Chanzo: [Calciomercato - in Italian]

Wasaka vipaji wa Manchester United na Newcastle wanafuatilia ukuzaji wa kiungo wa kati wa PSV Eindhoven na Uholanzi Xavi Simons, 19.

Chanzo: [Ekrem Konur]

Nottingham Forest bado hawajaamua iwapo watamsajili mlinda mlango wa Uingereza Dean Henderson, 26, au kipa wa Costa Rica Keylor Navas, 36, kwa mkataba wa kudumu baada ya kumalizika kwa uhamisho wao wa mkopo kutoka Manchester United na Paris St-Germain.

Chanzo: [Football Insider]

Chanzo: www.tanzaniaweb.live