Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI: Kocha mpya Singida FG asepa kimya kimya

Kocha Mpya Singida Ernst Middendorp, Kocha Mpya Singida FG

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mpya wa klab ya Singida Fountain Gate raia wa Ujerumani Ernst Middendorp (64) jana Mchana (Jumatatu) aliandika barua ya kung'atuka kikosini humo huku sababu ikiwa ni kuingiliwa na Viongozi klabuni hapo kwenye majukumu yake.

Mpaka muda huu Viongozi wa Juu wa klab ya Singida Big Stars wanahaha kujua alipo wakati Simu zake zote zikiwa zimezimwa (hapatikani).

Chanzo makini kimethibitisha kuwa, Kocha amechukizwa na Viongozi wake klabuni hapo kutaka kumpangia wachezaji wa kucheza Kwenye mchezo wao dhidi ya Future.

Juhudi za Kutaka kujua alipo zinaendelea ili wazungumze nae na arejee kwenye majukumu yake klabuni hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live