Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#TETESI: Kapombe, Chama na Inonga wasimamishwa Simba

Shomari Kapombe.png #TETESI: Kapombe, Chama na Inonga wasimamishwa Simba

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji watano wa Simba Sc akiwemo Henock Inonga, Cloutos Chama, na Shomary Kapombe wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi yao baada ya kufungwa na Yanga SC mabao 5-1 siku ya jumapili

Wachezaji hao wanatuhumiwa kuihujumu timu kitendo kilichopelekea kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao

Maamuzi hayo yamefanyika katika kikao cha bodi ya wakurugenzi ya Simba kilichofanyika jana jijini Daresalam

Chanzo cha uhakika kutoka Simba SC kimeiambia kishamba Media kuwa uongozi umeshapata ushahidi wa awali kuhusu tuhuma dhidi ya wachezaji hao na sasa imeanza uchunguzi wa kina ili kujiridhisha

Wachezaji hao watakua nje ya kambi ya timu mpaka hapo maamuzi mengine yatakapofanyika

Chanzo hicho kimesema huwenda leo klabu ya Simba ikatoa taarifa ya wazi kwa Umma juu ya maamuzi waliyofikia kuhusu wachezaji hao wau wasitoe ila wahusika wamepewa taarifa

Maamuzi mengine yaliyofikiwa na bodi ni kufutwa kazi kwa kocha mkuu Robertinho, msaidizi wake pamoja na kocha wa viungo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live