Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI: Joshua Kimmich awagonganisha vigogo Ulaya

Joshua Kimmich Furaha Joshua Kimmich

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester United ilituma maskauti kumtazama mshambuliaji wa Bologna Mholanzi Joshua Zirkzee katika mchezo wao dhidi ya Atalanta siku ya Jumapili.

Arsenal pia wana nia ya kumsajili Zirkzee, ambaye anaweza kugharimu kama €80m (£68m).

Manchester City wanajiandaa kuipiku Liverpool katika kumsajili kiungo wa kati wa Bayern Munich na Ujerumani Joshua Kimmich, 29, msimu huu.

Liverpool wanavutiwa sana na winga wa Wolves Pedro Neto mwenye umri wa miaka 23, lakini wana wasiwasi kuhusu rekodi ya jeraha ya mshambuliaji huyo wa Ureno.

Crystal Palace wanaandaa orodha ya wachezaji wanaolengwa wa nafasi ya mlinzi wa kati huku beki wa Uingereza Marc Guehi, 23, akitarajiwa kuuzwa msimu huu wa joto kwa ada ya zaidi ya £50m.

Kocha wa Sporting Lisbon, Ruben Amorim ndiye anayelengwa zaidi na Barcelona kurithi mikoba ya Xavi mwishoni mwa msimu huu, ingawa meneja huyo wa Ureno anaaminika pia kuwa na hamu ya kujiunga na Liverpool.

Bayern Munich wanavutiwa na mlinzi wa pembeni wa Bayer Leverkusen na Uholanzi Jeremie Frimpong, 23, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha kati ya €40m (£34.2m) na (£38.5m) €45m.

Newcastle wako kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 25 Lloyd Kelly kwa uhamisho wa bure.

Barcelona itasikiliza ofa kwa kiungo wa kati wa Uhispania Pedri, 21, msimu huu kwa sababu ya wasiwasi juu ya historia yake ya jeraha huku wakijaribu kusawazisha vitabu vyao.

Everton inamfuatilia mlinzi wa Hull City Jacob Greaves, 23, huku kukiwa na nia ya kumnunua beki wa kati wa England chini ya umri wa miaka 21 Jarrad Branthwaite, 21, kutoka Manchester United na Tottenham.

Vilabu vinne vya Premier League vinapigana vikumbo kumsaini Roony Bardghji wa Copenhagen mwenye thamani ya pauni milioni 20, huku Aston Villa, Newcastle, Tottenham na Manchester United zote zikimhitaji kiungo huyo wa kati wa Uswidi mwenye umri wa miaka 18.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live