Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI: Fei toto, Azam ni suala la muda tu

Fei Toto Kirumba Kiungo wa Yanga, Feisal Salum

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga SC, Feisal Salum (Fei Toto) huenda akatimkia kunako klabu ya Azam mwisho mwa msimu huu (2022/23) baada ya Azam kumuwekea mezani takribani Tsh. Milioni 350 kama pesa ya usajili.

Katika kuhakikisha wanainasa saini ya kiungo huyo Azam wapo tayari kutanguliza kishika uchumba ambapo kila mwezi Fei Toto atapokea Milioni 10 hadi dirisha kubwa la usajili litakapo funguliwa na kumwaga wino rasmi kuwatumikia matajiri hao wa jiji la Dar es Salaam.

Inasemekana Azam wamekubali kuuvunja mkataba wa Fei na Yanga ambapo watalipa milioni 100 na mshahara wa miezi mitatu kama masharti yaliyopo kwenye mkataba wake na Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live