Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI: Beki la CHAN laomba kusepa Yanga

Mamadou Doumbia Gh Mamadou Doumbia akiwa na Rais wa Yanga, Hersi Said

Mon, 27 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki Raia wa Mali Mamadou Doumbia anatajwa kuwa ameomba kuondoka katika klabu ya Yanga baada kuona ameshindwa kupata nafasi katika kikosi hicho kinachonolewa na Mtunisia Nasreddine Nabi.

Kumbe kitendo cha kukalishwa benchi, kinamuuma beki mpya wa Yanga, Mamadou Doumbia na sasa beki huyo inaelezwa amepanga kutuma maombi ya kutaka kuvunjwa mkataba ili aende sehemu ambayo itamfanya acheze kama ilivyokuwa kabla ya kutua Yanga.

Doumbia amejiunga na Yanga akitokea klabu ya Stade Malien ya nchini Mali Januari mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live