Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI: Azam wasaka mrithi wa Dabo

Abdihamid Moallin Azam Abdihamid Moallin

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa za uhakika zinasema Uongozi wa Azam FC, umetuma ofa kwa kocha mkuu wa KMC FC, Abdulhamid Moalin arejee kwa mara nyingine ndani ya viunga vya Azam Complex.

Azam FC ilishatuma ofa ya kwanza kwa Kocha Abdulhamid Moalin ambayo ameikataa baada ya kuwa na maslahi ambayo bila shaka Kocha Moalin ameona hakuna sababu ya kuiacha KMC FC ambayo inashika nafasi ya tatu kwenye ligi.

Baada ya Ofa ya Kwanza kukataliwa Azam FC imetuma ofa ya pili kwa Abdulhamid Moalin, Ofa ambayo bado hajaijibu mpaka muda huu,

Mpaka sasa ofa waliyotuma Azam FC kwenda ndabi ya klab ya KMC ni kama imepitishwa kwakuwa KMC hawana uwezo wa kumzuia kocha huyo na hata kumpa mahitaji hayo ambayo Azam Fc watampatia tena,

Inaelezwa viongozi wa KMC FC mpaka sasa bado hawaelewi wafanye nini Kwa maana Moalin kwa kipindi kifupi ndani ya KMC FC ametengeneza kikosi bora na cha ushindani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: