Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETES ZA USAJILI: Benfica wanataka Kitita kumuachia Nunez

Nunez.jpeg Darwin Nunez ana umri wa miaka 22

Sat, 4 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tetezi za usajili barani Ulaya kwa mara ya kwanza Manchester United wamepeleka ofa ya kumsajili Darwin Nunuez wa Benifica na Tottenham wamejitoa kwenye mbio za kumsajili Dybala kisa mshahara mkubwa.

Klabu ya Benifica ya nchini Ureno imeikataa ofa ya kwanza ya Manchester United ya Pauni million 80 walioiwasilisha kama ada ya uhamisho ya mshambuliaji Darwin Nunez.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Ureno inaripotiwa kuwa Benifica wapo tayari kumuuza mshambuliaji huyo raia wa Uruguay mwenye umri wa miaka 22 kwa ada ya Pauni milioni 88.8 ambayo ni zaidi ya 257,185,430,880. kwa pesa za kitanzania.

Kwingineko klaby ya Tottenham Hotspur ya England imejitoa kwenye kinyanganyiro cha kumuwania mshambuliaji Paulo Dybala ambaye atakuwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Juventus ya Italia kumalizika mwishoni mwa mwezi Juni.

Spurs walikuwa tayari kumsajili Dybala lakini mahitaji ya mshahara ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye miaka 28 ni makubwa. Dybala anataka mshahara wa pauni laki 280,000 kwa wiki ambayo ni zaidi ya Milioni 813 kwa pesa za kitanzania.

Klabu za Inter Milan ya Italia na Manchester United ya England nazo zinaripotiwa kuwa zimeonyesha nia yakumsajili Dybala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live