Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TBT: Unamkumbuka huyu mwamba?

Cambiasso.jpeg Esteban Cambiasso

Thu, 30 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unamkumbuka Esteban Cambiasso, kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina ambaye pia alipita katika vilabu vingi Kama River Plate,Real Madrid,Inter Milan, Leicester City na Olympiacos.

Cambiasso ama Cuchu Kama anavyopenda kujiita mwenyewe, alitamba sana akiwa na klabu ya Inter Milan kuanzia 2004 hadi 2014 na mafanikio makubwa zaidi katika career yake aliyapata akiwa hapo.

Esteban Cambiasso Deleau alikuwa miongo mwa wachezaji katika kikosi cha Inter Milan kilichoshinda treble (Serie A,Coppa Italia na Champions league) msimu wa 2009-10 chini ya Jose Mourinho.

nikukumbushe kidogo baadhi ya majina katika kikosi cha Inter Milan hiyo ya moto, alikuwepo mlinda mlango Julio César, Maicon, Iván Córdoba, Javier Zanetti, Lúcio, Thiago Motta, Ricardo Quaresma, Samuel Eto'o, Wesley Sneijder, McDonald Mariga, Mario Balotelli, Diego Milito na wengine wengi.

Esteban Cambiasso akiwa na Inter Milan

mechi 431 mabao 51 pasi za mabao 33 jumla ya mataji 15

Esteban Cambiasso (Cuchu) kwa sasa ni kocha msaidizi katika kikosi cha timu ya taifa ya Colombia, unamkumbuka kwa lipi mwamba huyu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live