Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TBC wazindua msimu wa pili Ligi Kuu

183080b02c0ee23de4bd5629aa472ba4 TBC wazindua msimu wa pili Ligi Kuu

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Wakati mechi ya Ngao ya Jamii ya watani wa jadi Simba na Yanga ikifanyika kesho, Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), limezindua msimu wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza kutimua vumbi Agosti 15 mwaka huu.

Mabingwa watetezi Yanga wataanza kutetea taji lao kwa kumenyana na Polisi Tanzania siku ya Jumanne Agosti 16, wakati mahasimu wao Simba watamenyana na Geita Gold Agosti 17.

Wapinzani hao wa jadi, kesho watashuka dimbani kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa ukiwa ni mchezo wa hisani wa Ngao ya Jamii kuashiria ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023 utakaofanyika saa moja usiku.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa TBC, Daphrosa Kimbory, amesema TBC ina mkataba wa miaka 10 na Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa, awamu ya kwanza ilikuwa ni msimu wa 2020/2021 na awamu ya pili ndio wamezindua leo ya 2022/2023

“Msimu wa kwanza umemalizika tunaingia msimu wa pili, awamu ya kwanza ni sehemu ya mafunzo, awamu hii tumejifunza jinsi ya kuboresha misimu ijayo, mwaka 2021/2022 TBC ilifanikiwa kutangaza michezo yote 240,” amesema na kuongeza:

“Tumesimika mitambo mipya katika mikoa mbalimbali, TBC inaendelea kuimarika hasa kwa wananchi wa mikoa ya pembezoni, tumeongeza usikivu kwa asilimia 83 nchi nzima, ” amesema.

Mkataba wa TBC wa kurusha matangazo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa miaka 10 una thamani ya Sh bilioni 3.54 na matangazo hayo yatarushwa kwa njia ya redio.

Chanzo: www.habarileo.co.tz