Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TBC mko wapi? Mnatafutwa huku Azerbaijan

TBC TAIFA TBC mko wapi? Mnatafutwa huku Azerbaijan

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ameandika Mchambuzi wa Soka, Jamedari Said;

"Jana jioni Taifa Stars ikiwa hapa Baku Mji Mkuu wa Jamhuri ya Azerbaijan ilifanya mazoezi kwenye kiwanja cha Olympic Stadium ambacho mwaka 2019 kiliandaa fainali ya UEFA EUROPA LEAGUE ambapo Chelsea “The Pride of London” tuliishi na Arsenal “The Gunners” na tukawachapa bao 4-1 hapa kwenye kiwanja hiki.

"Jana tukiwa hapa Stars wanafanya mazoezi nikakutana na mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni ya Taifa ya Bulgarian (swipe) akawa anataka kufahamu baadhi ya mambo kuhusiana na Stars. Tayari alikuwa na chapisho la TFF ambalo lilikuwa na majina ya wachezaji walioitwa kwenye timu.

"Akawa anahoji kuhusiana na wachezaji waliopo na ambao hawajafika, akaomba nimfundishe kutamka majina ya Kitanzania kwani yeye atatangaza hiyo mechi kati ya Tanzania na Bulgaria kwenye televisheni ya Taifa lao, yani kama TBC ya kwetu Tanzania. Akataka kujua mimi ni nani kwenye timu nikamuambia ni mwandishi wa habari kama yeye, akauliza wa kituo cha Taifa (TBC)?

"Nikamjibu hapana ni kutoka chombo binafsi na nikamuambia hata hao unaowaona wengine hawatoki televisheni ya Taifa kama wewe, wote ni vyombo binafsi tu.

"Akashangaa kiasi akauliza kama Televisheni ya Taifa haiwezi kuja kuonyesha mechi za timu ya Taifa kinafanyaje majukumu yake? Nikamjibu sijui kwakuwa mimi sifanyi kazi huko kwao.

"Sema akanikumbusha tu kwamba sijawaona TBC kwenye safari za timu za Taifa au hata mapokezi kwa muda mrefu, nakumbuka hata Stars walipotoka kufuzu kwajili ya AFCON pale JNIA sikuwaona pia, lakini kwakuwa hayanihusu nikaacha yapite.

Ila jamaa kashangaa sana kwa chombo cha utangazaji cha Taifa kutokuwepo kwenye tukio kama hili la timu ya Taifa ambayo ni nembo ya Taifa pia."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live