Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANZIA: Silvio Berlusconi afariki Dunia

Silvio Berlusconi, Silvio Berlusconi

Mon, 12 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa zamani wa AC Milan ambaye pia alihudumu kama Waziri Mkuu wa Italia, Silvio Berlusconi, amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 86.

Silvio amefariki katika hospitali ya San Raffaele Jijini Milan ambapo alikuwa akipokea matibabu baada ya kukutwa na maambukizi ‘infection’ kwenye mapafu.

Hii ni kutokana na kuwahi kukutwa na ugonjwa wa Leukaemia sugu ambayo ni aina ya saratani inayoathiri seli nyeupe za damu na uboho wa mfupa.

AC Milan walifanikiwa kutwaa mataji 29 ndani ya miaka 31 ambayo alihudumu kama Rais na mmiliki wa Klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live