Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANZIA: Mwanasoka wa zamani wa Ligi Kuu England afariki

IMG 4453.jpeg Mshambuliaji wa zamani wa Ubelgiji, Cedric Roussel

Sun, 25 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa zamani wa Ubelgiji, Cedric Roussel amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 45 baada ya kupata mshtuko wa moyo.

Roussel alianza maisha yake ya soka Nchini kwao Ubelgiji kabla ya kujiunga na Coventry almaarufu Sky Blues kwa mkopo kutoka Gent mwaka 1999 na baadae alijiunga jumla na Coventry ambapo alikudumu nao mwaka mmoja kabla ya kutimkia Wolves.

Kupitia taarifa yake kwa umma klabu ya Coventry City imesema "Coventry City ina huzuni kubwa kusikia kifo cha mshambuliaji wetu wa zamani Cedric Roussel, akiwa na umri wa miaka 45 tu.

Kwa upande wake timu ya Taifa Ubelgiji kupitia taarifa yake Twitter imesema "Tunatuma salamu zetu za pole kwa familia na marafiki wa Cedric Roussel."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live