Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANZIA: Mke wa Sir Alex Ferguson afariki Dunia

Skysports Sir Alex Ferguson 6311221 Sir Alex Ferguson akiwa na Mkewe

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mke wa Sir Alex Ferguson, mrembo Cathy amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84.

Mke huyo wa kocha wa zamani wa Manchester United alifariki asubuhi ya leo Ijumaa huko Cheshire.

Taarifa ya familia ya Ferguson ilifichua: "Kwa huzuni kubwa tunathibitisha kifo cha mama Cathy Ferguson kilichotokea leo akiwa ameacha mume, watoto na wajukuu 12 na kitukuu mmoja."

Ferguson na mkewe walioana karibu miaka 60 iliyopita. Cathy alikutana na Sir Alex, 81, mwaka 1964 wakati kocha huyo alipokuwa na umri wa miaka 23 na walifunga ndoa mwaka 1966.

Wawili hao wamebahatika kupata watoto watatu wa kiume - Mark, aliyezaliwa 1968, na pacha Darren na Jason, waliozaliwa 1972 - na wajukuu 12.

Katika nyakati alizopewa utulivu mkubwa na mkewe, Ferguson ameweza kushinda mataji 38, ikiwamo 13 ya Ligi Kuu England na mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live