Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANZIA: Kocha Nabi afiwa na Baba yake

Nasreddine Nabi Msiba Nasreddine Nabi

Sat, 11 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa aliyewahi kuwa Msemaji wa Yanga, Haji Manara ametutaarifu kuwa Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga ambae kwa sasa anafundisha Klabu ya FAR Rabbat ya nchini Morocco, Nasreddine Nabi amefiwa na Baba yake leo Novemba 11.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Manara ameandika;

"Nimepokea Taarifa sasa hivi Kocha wetu zamani wa Yanga Professor @nabinasreddine amefiwa na Baba yake Mzazi huko Monastir nchini Tunisia Asubuhi ya leo.

Nimeongea na Kocha Nabi Mchana huu pamoja na Bernard Morrison @bm3gh kunipa taarifa hizi ili niwajulishe Watanzania na Washabiki wetu ambao walikaa na Kocha Nabi vzuri mno!

Kwa leo Nabi hatakaa jukwaani team yake itakapokuwa ikicheza mechi ya ligi na tayari maandalizi ya kwenda kwao Tunisia kuwahi msiba yanaendelea.

Kwa niaba yenu nimempa pole nyingi Kocha wetu ambae amejawa na huzuni ya kumpoteza Baba yake"

Tanzaniaweb Tunatoa pole kwa familia ya Kocha Nabi na mungu ampe ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: