Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANZIA: Kipa wa zamani Taifa Stars afariki Dunia

Difu Afariki Dunia.jpeg Difu (katikati) alizichezea timu kama Cosmopolitan

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa kipa wa Cosmopolitan, mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania mwaka 1967, Mohamed Mfaume ‘Difu’ (katikati) amefariki dunia Ijumaa ya Aprili 14 Jijini Dar es Salaam.

Kipa wa timu ya taifa ya Tanzania pia kuanzia miaka ya 1960 hadi 1970 mwanzoni anatarajiwa kuzikwa leo makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.

Mfaume Difu alikuwa kipa wa Cosmopolitan wakati inachukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania mwaka 1967, kabla ya kuifikisha Bara Fainali ya Kombe la Challenge mwaka 1970 ambako ilifungwa na Uganda.

Mohamed Mfaume ‘Difu’ pia alikuwa mmoja kati ya wanasoka wasomi nchini ambaye alikuwa Afisa mkubwa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mungu ampumzishe kwa amani mlinda mlango Mohamed Mfaume ‘Difu’. Amin

Chanzo: www.tanzaniaweb.live