Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANZIA: Katibu Mkuu wa zamani TFF afariki dunia

Katibu Mkuu Afariki.jpeg Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ashery Gasabile

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Ashery Gasabile amefariki Dunia leo Aprili 27, 2023 jijini Mwanza.

TFF kupitia barua yake kwa umma imetuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huo.

“Marehemu Gasabile atakumbukwa kwa mchango wake kwenye maendeleo ya mpira wa miguu. Alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza baada ya mabadiliko kutoka Chama Cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT), na kuwa TFF.” TFF

“TFF inaungana na wafiwa katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mpendwa wao.”

“Gasabile wakati wa uhai wake aliongoza katika wadhifa wa ngazi mbalimbali ikiwemo wadhifa wa Katibu Mkuu wa TFF.” - TFF

Mungu ailaze roho ya marehemu Ashery Gasabile mahala pema, Amina.

Shirikisho la Soka nchini TFF latoa pole, Tazama taarifa hapa chini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live