Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#TANZIA: Ally Sonso afariki Dunia

Sonso Ally Mtoni Sonso

Fri, 11 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sentahafu wetu wa zamani wa Klabu ya Yanga Ally Mtoni Sonso amefariki dunia leo kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kwa Taarifa zaidi juu ya taratibu za mazishi, endelea kuwa karibu na Tanzania Web ambapo tutakujuza kwa kila taarifa zitakavyokuwa zikitufikia.

Sonso anakumbukwa kwa mengi ikiwemo ujasiri wake ndani ya Uwanja, nidhamu pamoja na kujitolea kuipigania jezi ya timu yake uwanjani.

Tunamuombea kwa Mungu aipokee roho ya mpendwa wetu Ally na pia Tanzania Web tunatoa pole kwa wafiwa wote, hususan familia yake.

Katika kipindi cha Uhai wake, Sonso amepata kuvichezea vilabu vya Lipuli FC, Yanga SC, Kagera Sugar, Polisi Tanzania pia amewahi kucheza timu ya Taifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live