Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sven kuweka silaha sawa leo

Sven Pic Data Sven kuweka silaha sawa leo

Sun, 10 Jan 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Thomas Ng'ituMore by this Author Dar es Salaam. Kocha wa Simba, Sven Vandebroeck ataweka wazi jeshi lake litakaloizamisha FC Platnum katika mchezo wa Jumatano wa Ligi ya Mabingwa Adria.

Mabingwa watetezi wana kibarua cha kupindua matokeo dhidi ya miamba hiyo ya Zimbabwe baada ya mchezo wa awali kukubali kipigo cha bao 1-0 mjini Harare.

Ili kusonga mbele, Simba inahitaji ushindi wa mabao 2-0 au zaidi kujihakikishia kutinga katika hatua ya makundi ya mashindano hayo makubwa Afrika katika ngazi ya klabu.

Mchezo huo wa marudiano unatarajiwa kufanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, keshokutwa, wakati mashabiki wakiongeza presha kwa kocha Sven kutaka matokeo mazuri kama ilivyokuwa kwa misimu miwili iliyopita.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz