Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sven apewe Timu Liverpool atimize ndoto yake

Sven Concup Sven apewe Timu Liverpool atimize ndoto yake

Mon, 15 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wa Liverpool wameitaka klabu hiyo kumuwezesha Kocha mkongwe Sven-Goran Eriksson (75),kutimiza ndoto yake ya kuwa Meneja wa klabu hiyo kwa mechi moja.

Akihojiwa na Sky News, Meneja huyo wa zamani wa England, ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa Saratani alimueleza Mtangazaji kuwa jambo pekee analojutia ni kutokuwa Meneja wa Liverpool.

Baada ya mahojiano hayo, mdau mmoja wa mtandao wa YouTube aliyejikita kwenye masulala ya soka alitoa wazo la kumpa nafasi Sven kusimamia mechi ya wakongwe wa Liverpool inayotarajia kuchezwa mwezi Machi dhidi ya Ajax.

Mashabiki wengi wa Liverpool wameonekana kuunga mkono wazo hilo.

Mechi hiyo ya hisani ambayo huchezwa mara moja kwa mwaka hulenga kukusanya fedha za misaada kwa watoto na vijana.

Sven anasumbuliwa na Saratani ya kongosho ambayo ipo kwenye hatua za mwisho na taarifa za kitabibu zimekadiria kuwa amebakiza takribani mwaka mmoja wa kuishi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live